Mchezaji
wa zamani wa timu ya taifa ya italia anaekipiga kunako klabu ya AS Roma
FRANCESCO TOTTI amesema hafikirii kustaafu soka kwa sasa ingawa hana furaha na
mchezo kama ilivyokuwa zamani kutokana na wachezaji wa kisasa kitumia nguvu
nyingi.
Mshambuliaji
huyo mwenye miaka 37 aliyeitumikia AS ROMA tangu mwaka 1993 na ameichezea klabu
hiyo zaidi ya mechi 650, amesema nikweli anaelekea kwenye utu uzima lakini bado
ana kiwango kizuri kuliko wachezaji wenye umri mdogo.
Aidha
mkongwe huyo aliyeifungia ROMA magoli 26 msimu uliopita amesema mambo
yamebadilika kunako klabu hiyo na anaandika kitabu kuhusu marais, makocha na
wachezaji wote walioingia na kutoka katika klabu hiyo tangu ajiunge nayo mwaka
1993.


No comments:
Post a Comment