Thursday, August 28, 2014

VAN GAAL : SITISHIKI NA KIPIGO CHA MK DONS,NIPENI MUDA KIDOGO

                                                                     Van Gaal hana mawazo mapya



Kocha wa Manchester United LOUIS VAN GAAL amewaudhi wapenzi wa klabu hiyo baada ya kusema kuwa hakushangazwa na kichapo cha mabao 4-0 mikononi mwa klabu dhaifu ya MK DONS iliyo katika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi   daraja la kwanza katika mechi ya kuwania ubingwa wa kombe la Capital One .



Kocha huyo alisema kuwa timu haijengwi kwa mwezi mmoja hivyo anahitaji muda kidogo akiwa kama kocha wa timu hiyo ili kuweka mambo sawa na Kufuatia kipigo hicho kocha huyo raia wa uholanzi  ameongeza nguvu zake kwa kiungo wa klabu ya juventus ARTURO VIDAL kwa kutoa ofa ya paundi milioni 33.4 ili kupata huduma ya mchezaji huyo kutoka nchini chile.



United tayari wametumia zaidi ya paundi milioni 132 katika usajili baada ya kutoa paundi milioni 59.7 kumnunua ANGEL DI MARIA kutoka Real Madrid na bado wanataka kuongeza wachezaji kabla dirisha la usajiri kufungwa siku ya jumatatu ili kuepusha maandamano yaliyopangwa kufanywa na mashabiki wa klabu hiyo kutokana na mwenendo mbovu wa klabu yao..

No comments:

Post a Comment