Yanga wakiwa Mazoezini pamoja na Cotinho,Jaja
KOCHA Mkuu wa Yanga SC,
Mbrazil Marcio Maximo amewaambia wanachama na wapenzi wa timu hiyo, wawavutie
subira wachezaji wapya waliosajiliwa ili wazoee na kuanza kufanya vitu.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mchana wa leo, makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es
Salaam, Maximo amesema wachezaji Wabrazil wenzake, kiungo Andrey Coutinho na
mshambuliaji Geilson Santana Santos ‘Jaja’ wote ni wazuri.
“Hawa wachezaji wapya wa
Brazil wote ni wazuri, Coutinho na Jaja wataisaidia timu, mashabiki na wapenzi
wawape muda, waache kuwazomea,”amesema Maximo.
Maximo
alikuwa akizungumzia mchezo wa kirafiki wa Jumapili dhidi ya Bata Bullets ya
Malawi, ambao amesema utakuwa wa mwisho kabla ya kumenyana na Azam FC katika
mechi ya Ngao ya Jamii Septemba 14.
Amesema
baada ya mechi hiyo, timu yake itaingia kambini kujiandaa na mchezo wa Ngao
dhidi ya Azam FC, ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara.
Tayari
Yanga SC imekwishacheza mechi nne za kujipima chini ya Maximo tangu aanze kazi
Julai na kushinda zote, 1-0 mara mbili dhidi ya Chipukizi ya Pemba na Thika
United ya Kenya na 2-0 pia mara mbili dhidi ya Shangani na KMKM zote za
Zanzibar. Coutinho na Jaja wote wamefunga mabao mawili kila mmoja katika mechi
hizo nne.
No comments:
Post a Comment