Mchezaji mpya wa Manchester United aliyesajiliwa kwa dau
la kuvunja rekodi msimu huu, Angel Di Maria,ameonesha kile atakachoifanyia
klabu yake hiyo mpya,baada ya jana usiku kutengeneza nafasi tatu zilizozaa
magoli na mwenyewe kutumbukiza la kwake,wakati Argentina ikilipa kisasi kwa Ujerumani
kwa kuitandika mabao 4-2.
Di Maria,aliyesajiliwa kwa kitita cha pauni milinoni 59.7,alianza makeke
yake kwa kutengeneza pasi kwa Sergio Aguero,aliyekwenda kufunga bao la kwanza
katika dakika ya 20,kabla ya kumtengenezea pasi nyingine Erik Lamela,aliyefunga
bao la pili katika daika ya 40.
Hali hiyo ikazidi kumchanganya kocha wa Ujerumani Joachim Low,ambaye
aliingia uwanjani kutaka kuendeleza ubabe kwa Argentina baada ya mwezi julai
kuifunga bao 1-0 katika fainali ya kombe la dunia huko Brazil,lakini mambo
hayakuwa kama alivyofikiria.
Katika dakika ya 48 Di Maria akafanya kazi nzuri nyingine kwa kumpa pasi
yenye manufaa Fernandez,aliyefunga bao la tatu,na alipoona amechoka kutoa pasi
kwa wenzake akaamua kutumbukiza mwenye bao la 4 katika dakika ya 50,kabla ya
mchezaji wa Chelsea Andre Schurrle na Mario Gotze kuipatia Ujerumani mabao 2
katika dakika ya 52 na 78.
………………………………………………………………………………VIKOSI KAMILI KATIKA MCHEZO HUO
Germany
- 01 Neuer (Weidenfeller - 45' )
- 15 Durm
- 02 Großkreutz
- 03 Ginter
- 04 Höwedes (Rüdiger - 77' )
- 21 Reus
- 18 Kroos (Rudy - 71' )
- 24 Kramer
- 09 Schürrle (Müller - 57' )
- 14 Draxler Booked (Podolski - 33' Booked )
- 23 Gomez (Götze - 58' )
Substitutes
- 05 Hummels
- 07 Rudy
- 10 Podolski
- 12 Zieler
- 13 Müller
- 19 Götze
- 20 Boateng
- 22 Weidenfeller
Argentina
- 01 Romero (Andujar - 80' )
- 04 Zabaleta (Campagnaro - 77' )
- 16 Rojo
- 15 Demichelis Booked
- 17 Fernández
- 06 Biglia
- 14 Mascherano
- 08 Pérez (Fernández - 45' )
- 10 Agüero (Gaitán - 83' )
- 18 Lamela (Gago - 68' )
- 07 Di María (Álvarez - 86' )
Substitutes
- 03 Campagnaro
- 05 Gago
- 09 Higuaín
- 13 Fernández
- 19 Álvarez
- 20 Gaitán
- 21 Andujar
- 22 Lavezzi
- 23 Basanta

No comments:
Post a Comment