Saturday, September 6, 2014

BAADA YA KUAIBISHWA KWENYE KOMBE LA DUNIA,NEYMAR AIFUTA MACHOZI BRAZIL





                                                 Neymar akipongezwa baada ya kuing'arisha Brazil
MSHAMBULIAJI Neymar,amefunga goli pekee zikisalia dakika 7 mpira kwisha,mbele ya kocha mpya wa Brazil,Dunga,akiisambaratisha Colombia iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani baada ya mmoja kuzawadiwa kadi nyekundu.

Mshambuliaji huyo wa Barcelona,alifunga bao hilo kwa mkwaju huru na kuifanya Brazil waliokuwa nyumbani kuandika ushindi wa kwanza tangu walipomaliza katika nafasi ya nne kwenye michuano ya kuwania kombe la dunia iliyomalizika nchini mwao.

Colombia walisalia wachezaji 10 katika ilipofika dakika ya  49,baada ya mchezaji wao, Juan Cuadrado ,kutolewa nje na mwamuzi kwa kucheza rafu.

Katika mchezo huo,mshambuliaji mpya wa Manchester United Radamel Falcao aliyeanzia benchi ,alishindwa kuonesha makeke yake na kujikuta akucheza kwa muda wa dakika 13 tu wa Colombia kuamua kumtoa nje.

VIKOSI VYA MCHEZO HUO JANA


Brazil

  • 01 Jefferson
  • 06 Filipe Luis
  • 04 David Luiz (Marquinhos - 80' )
  • 03 Miranda
  • 02 Maicon
  • 17 Luiz Gustavo Booked (Fernandinho - 45' )
  • 19 Willian (de Barros Ribeiro - 72' )
  • 11 Oscar (Coutinho - 72' )
  • 08 Ramires Booked (Mendes Trindade - 45' )
  • 10 Neymar
  • 09 Tardelli (Robinho - 77' )

Substitutes

  • 05 Fernandinho
  • 07 Robinho
  • 12 Barbosa
  • 13 Marquinhos
  • 14 Nascimento Silva
  • 15 Marcelo
  • 16 Danilo
  • 18 de Barros Ribeiro
  • 20 Goulart Pereira
  • 21 Coutinho
  • 22 Mendes Trindade

Colombia

  • 01 Ospina
  • 18 Zuñiga Booked (Mejía - 73' )
  • 02 Zapata
  • 23 Valdés Booked
  • 07 Armero
  • 05 Leão Ramírez (Arias - 45' )
  • 10 Rodríguez (Falcao - 77' )
  • 06 Sánchez Booked (Ramos - 85' )
  • 11 Cuadrado Dismissed after an earlier booking
  • 21 Martínez (Guarín - 65' )
  • 19 Gutiérrez Booked (Bacca - 65' )

Substitutes

  • 04 Arias
  • 08 Aguilar
  • 09 Falcao
  • 12 Vargas
  • 13 Guarín
  • 15 Quintero
  • 16 Balanta
  • 17 Bacca
  • 20 Ramos
  • 22 Muriel
  • 24 Ibarbo
  • 25 Mejía
  • 26 Carbonero


STURRIDGE:NIMEVUNJIKA MOYO KUTOITUMIKIA ENGLAND





                                                                          Sturridge
Mshambuliaji Daniel Sturridge,amesema amevunjika moyo baada ya kutupwa nje ya kikosi cha England kitakachocheza mechi yake ya ufunguzi wa patashika ya kufuzu kutinga fainali za Euro 2016 dhidi ya Switzerland keshokutwa jumatatu.

Sturridge, 25,atakuwa nje ya kikosi hicho chini ya kocha Roy Hodgson,baada ya kuumia jana ijumaa wakiwa katika mazoezi na klabu yake ya Liverpool kwenye dimba la St George'Park.

Chama cha soka cha Uingereza FA,kimethibitisha kuwa mchezaji huyo wa Liverpool ataukosa mchezo huo wa kufuzu utakaopigwa mjini Basel.

"kusema kweli nimevunjika sana moyo kuona sitalitumikia taifa langu kwenye mchezo huo,lakini kwa mujibu wa madaktari-nina matumaini ya kurejea uwanjani muda mfupi tu ujao kushirikiana na wenzangu katika mechi zinazofuata,Ni maneno aliyoyaandika Sturridge kwenye mtandao wa kijamii wa Tweeter.

SINA FURAHA KUONA SIITUMIKII KLABU YANGU

                                               Suarez na mahojiano ya waandishi wa habari


Mshambuliaji mpya wa klabu ya fc Barcelona ya nchini Hispania LUIS SUAREZ amesema amekuwa na wakati mgumu kuitazama timu yake hiyo ikicheza pasipo kutoa msaada wake uwanjani.

SUAREZ hawezi kuitumikia timu hiyo kutokana na adhabu aliyopewa na shirikisho la soka duniani FIFA baada ya kumng’ata meno beki wa timu ya taifa ya italia GIORGIO CHIELLINI katika mashindano ya kombe la dunia 2014 nchini brazil.

Aidha mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 aliyetokea Liverpool atakuwa nje ya uwanja mpaka October 25,na amesema itamlazimu kuwa mvumilivu kwa kipindi hiki.

NITAIDAKIA TIMU YANGU YA CHELSEA KWA MUDA MREFU



Golikipa namba moja wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya ubelgiji THIBAUT COURTOIS amesema anataraji kusaini mkataba mpya atakaporejea katika klabu yake baada ya mechi za kimataifa kumalizika.

COURTOIS ambaye aliitumikia klabu ya atletico madridi ya nchini Hispania kwa misimu mitatu kwa mkopo amerejea katika klabu yake msimu huu na kuonesha kiwango cha hali ya juu na kumuweka benchi golikipa mkongwe wa klabu hiyo PETER CECH

Aidha kocha JOSE MOURINHO amesema anataraji kumpa mkataba wa miaka mitano Courtois, mwenye umri mdogo baada ya kuonesha kiwango kizuri katika mechi alizocheza.



KOCHA ENGLAND ATETEA KIKOSI CHAKE

                                        kocha Roy akiwapa maelekezo wachezaji wake


Kocha wa timu ya taifa ya England ROY HODGSON amewatetea wachezaji wa timu hiyo kutokana na mchezo mbovu waliuonesha katika mechi ya kirafiki baina ya timu hiyo na timu ya taifa ya Norway uliopigwa katika uwanja wa wembley na timu hiyo kuibuka na ushindi wa goli moja kwa bila.
HODGSON alichukia baada ya kuulizwa kwanini timu hiyo ilipiga mashuti mawili tu yaliyolenga goli na kujibu kuwa timu hiyo umeundwa na wachezaji wengi wasio na uzoefu hivyo haiwezekani mchezaji alieitumikia timu hiyo kwa mechi 4 mpaka 5 afanye makubwa kama aliyoyafanya DAVID BECKHAM na mchezaji majeruhi kama PHIL JONAS kumfananisha na mkongwe kama JOHN TERRY.
Aidha kocha huyo amesema anajua kuwa idadi ya mashabiki wa taifa hilo inapungua kila siku lakini yeye anachojali nikuhakikiksha timu hiyo inafanya vizuri na atahakikisha wanashinda mechi yao dhidi ya Switzerland jumatatu ijayo.